01 / 03
Mteja
Tembelea maduka na wamachinga wa Kariakoo, linganisha bei na agiza kwa urahisi kutoka kwenye simu yako.
- 01Agiza na ulipe ukipokea
- 02Fuatilia oda yako hatua kwa hatua
- 03Pata risiti halali ya kila manunuzi
Soko la Kariakoo, mfukoni mwako
Karia inakuunganisha na maduka na wamachinga wa kweli wa Kariakoo - tafuta bidhaa, ongea na muuzaji, na lipa ukipokea.
Kariakoo ni moyo wa biashara Tanzania. Sasa uko kwenye simu yako - tafuta bidhaa, linganisha bei, ongea na muuzaji na uletewe mlangoni.
Makundi ya bidhaa
Njia za kujiunga
TSH kwa mteja kutumia Karia
Nafasi kwa kila mtu
01 / 03
Tembelea maduka na wamachinga wa Kariakoo, linganisha bei na agiza kwa urahisi kutoka kwenye simu yako.
02 / 03
Fungua duka lako mtandaoni, weka bidhaa zako na wafikie wateja wapya kila siku bila gharama za fremu nyingine.
03 / 03
Tangaza unachouza mtaani, wafikie wateja wapya na weka kumbukumbu sahihi za mauzo yako.
Kila kitu Kariakoo
Kuanzia simu hadi vyakula, nguo hadi vifaa vya ujenzi - Kariakoo ina kila kitu.
Programu
Muundo rahisi na wa haraka, kwa Kiswahili na Kiingereza - ili kila mtu atumie kwa urahisi, hata kwa data kidogo.
Tumia Karia sasa


Kununua kwenye Karia
Tafuta bidhaa yoyote au pitia makundi.
Chagua idadi na anwani ya kuletewa.
Muuzaji anakuletea - lipa kwa pesa taslimu ukipokea.
Thibitisha umepokea na upate risiti yako.
Anza leo
Ingia au jisajili moja kwa moja hapa - inafanya kazi kwenye simu yoyote, iPhone au kompyuta. Huna haja ya kupakua chochote.
Pakua programu ya Karia kwa simu za Android - akaunti ni ileile, tumia popote.
Android pekee · Bure
Maswali
Ndiyo. Bonyeza "Tumia Karia sasa" na uingie au ujisajili moja kwa moja kwenye wavuti - kwenye simu yoyote au kompyuta. Akaunti ni ileile kama kwenye programu.
Hapana, Karia ni bure kabisa kwa wateja. Wenye maduka hulipa TSH 25,000 kila siku 30 (siku 30 za kwanza ni bure), na wamachinga hulipa TSH 500 kwa kila bidhaa wanayoweka.
Programu ya Karia ni kwa simu za Android. Kwenye iPhone na kompyuta, tumia Karia moja kwa moja kwenye wavuti - kwenye iPhone unaweza kuiweka kwenye Skrini ya Nyumbani ikae kama programu.
Unalipa kwa pesa taslimu pale bidhaa inapokufikia. Ukithibitisha kuwa umepokea, unapata risiti yako kwenye programu.
Kuhusu Karia
Karia ni programu iliyojengwa Tanzania kuleta soko maarufu la Kariakoo mtandaoni - ikiwasaidia wateja kununua kwa urahisi, na wenye maduka na wamachinga kufikia wateja wengi zaidi.